عربي - Arabic English Qafár af - Afar Afrikaans - Afrikanns Akan Shqip - Albanian አማርኛ - Amharic Հայերեն - Armenian অসমীয়া - Assamese Azərbaycanca - Azerbaijani Bamanankan - Bambara Bassa Bemba বাংলা - Bengali Bosanski - Bosnian Български - Bulgarian မြန်မာဘာသာ - Burmese Bisaya - Cebuano Cham Нохчий - Chechen chiCheŵa - Chewa 中文 - Chinese Адыгэбзэ - Circassian Hrvatski - Croatian Česky - Czech Dagbani Dansk - Danish فارسی دری - Dari Dendi ދިވެހި ބަސް - Dhivehi Nederlands - Dutch إستوني - Estonian Suomi - Finnish Français - French Fulfulde - Fula ქართული - Georgian Deutsch - German Ελληνικά - Greek ગુજરાતી - Gujrati Kreyòl ayisyen - Haitian Creole Hausa हिन्दी - Hindi Magyar - Hungarian Igbo Indonesia - Indonesian Italiano - Italian 日本語 - Japanese Jóola - Jola ಕನ್ನಡ - Kannada Қазақша - Kazakh ភាសាខ្មែរ - Khmer Kikuyu Ikinyarwanda - Kinyarwanda Ikirundi - Kirundi 한국어 - Korean كوردی سۆرانی - kurdish كوردي kurmancî - Kurmanji Kyrgyz ລາວ - Lao latviešu - Latvian Lingala lietuvių - Lithuanian Luganda Македонски - Macedonian Maguindanaon Malagasy - Malagasy Bahasa Melayu - Malay മലയാളം - Malayalam Mandinka मराठी - Marathi Mõõré - Moore नेपाली - Nepali أنكو - NKo Norwegian ଓଡ଼ିଆ - Odia oromoo - Oromo پښتو - Pashto فارسی - Persian Polski - Polish Portuguese ਪੰਜਾਬੀ - Punjabi Română - Romanian Русский - Russian Српски - Serbian Shona සිංහල - Sinhala Slovenščina - Slovenian Soomaaliga - Somali Soninke Sesotho - Sotho Español - Spanish Kiswahili - Swahili Svenska - Swedish Tagalog Тоҷикӣ - Tajik தமிழ் - Tamil తెలుగు - Telugu ไทย - Thai ትግረኛ - Tigrinya Türkçe - Turkish Ukrainian اردو - Urdu ئۇيغۇرچە - Uyghur Ўзбек - Uzbek Việt Nam - Vietnamese Wolof Yao Yorùbá - Yoruba Zarma زولو - Zulu
839 Hadithi
Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii
Makundi
Daraja la hadithi
Imesimuliwa katika
Msimulizi
Siku moja alisimama kwetu sisi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akatupa mawaidha makali mno, nyoyo zilisisimka kwayo, na macho yalibugujikwa machozi, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Umetuwaidhi mawaidha ya mwenye kuaga, tuachie usia. Akasema: " Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi, basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa (watawala) waongofu, zing'ateni (mzikamatilie) kwa magego, na tahadharini sana na mambo ya kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotevu".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Hakika nitampa bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu ataleta ufunguzi kupitia mikono yake". Akasema Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- sikuwa napenda uongozi wakati huo, fikra zikanipelekea kuwa na matarajio ya kuitwa kwa ajili ya bendera hiyo, akamuita Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Ally bin Abii Twalib -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akampa bendera hiyo, na akasema: "Nenda na usigeuke mpaka Mwenyezi Mungu akufungulie" Akatembea Ally mwendo kidogo kisha akasimama na wala hakugeuka kisha akazungumza kwa sauti ya juu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa lipi niwapige watu? Akasema: "Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wakifanya hivyo watakuwa wamekinga kwako damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki yake, na hesabu yao iko juu ya Mwenyezi Mungu".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Ninawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikia na utii, hata kama atakutawaleni mtumwa. Kwani hakika yeyote kati yenu atakayeishi, ataona tofauti nyingi. Kwa hivyo shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wanyoofu waongofu, zikamateni na kuzing'ata kwa magego. Na jihadharini na mambo ya kuzushwa. Kwani kila jambo jipya (katika dini) ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu."
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy
Ya kwamba siku moja alikuja katika jiwe jeusi akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama nisingemuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa siku tano naye akisema: "Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani, na lau kama ningelijifanyia mwandani katika umma wangu basi ningemfanya Abubakari kuwa mwandani, tambueni kuwa; Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na wema wao kuwa misikiti, tambueni vyema (kuweni makini)! yakuwa Msijelifanya kaburi langu kuwa msikiti, hakika nakukatazeni msifanye hilo".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Alisema kuhusu maanswari (watu wa Madina): Hawampendi ila mtu muumini, na hawamchukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- siku moja alimkosa Thabiti bin Kaisi, mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi naweza kukupa taarifa zake, akamfuata akamkuta akiwa amekaa nyumbani kwake, akiwa ameinamisha kichwa chake, akasema: Ni jambo gani limekusibu? Akasema: Ni shari, alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, tayari yameporomoka matendo yake, naye ni katika watu wa motoni, akarudi yule bwana kwa Mtume akamweleza kuwa kasema kadhaa wa kadhaa, mara ya pili akarudi kwake akiwa habari njema, akasema: "Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni, bali ni katika watu wa peponi".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Karne bora ni karne yangu, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata" Amesema Imrani: Sijui alitaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadaye karne mbili au tatu, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika baada yenu kutakuja watu wanaofanya hiyana na wala hawaaminiwi, na wanatoa ushahidi na wala hawatakwi ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na utadhihiri kwao unene".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake